Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imesema itaendelea kuhakikisha miradi ya mazingira katika maeneo mbalimbali nchini inatekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa ili iwanufaishe wananchi na kutatua changamoto za kimazingira.

Pia, imesema itashirikiana na Wizara nyingine za kisekta kuona namna namna bora ya kuvuna maji ili kudhibiti mafuriko yanaoyakumbuka maeneo mbalimbali nchini na kusababisha adha kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis leo Aprili 19, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Serengeti Jeremiah Mrimi.

Katika swali la msingi Mhe. Mrimi alitaka kujua mpango wa Serikali wa kudhibiti mafuriko katika Mto Mara kwa kuvuna maji yake kupitia mabwawa na kujenga skimu za umwagiliaji.

Akiendelea kujibu swali hilo, Khamis amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais ina utaratibu wa kutembelea na kukagua miradi inayoratibiwa na Ofisi hiyo na kutoa maelekezo ikamilike kwa wakati na kwa kiwango.

Amebainisha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais tayari imezindua Mpango Kabambe wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032) ambao umeelezea mikakati na shughuli endelevu zinazoweza kufanyika ili kuhifadhi mazingira.

Mpango Kabambe wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022- 2032) ulizinduliwa Juni 05, 2022 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati wa kilele cha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma.

Ajali ya gari yachukua uhai wa Mwandishi Morogoro
Osimhen atajwa FC Bayern Munich