Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amekasirishwa na kitendo cha Mradi wa Maji Kazuramimba kuchukua muda mrefu bila kukamilika wakati wananchi wakiendelea kuteseka na ukosefu wa huduma hiyo muhimu ambapo awali changamoto ilikua ni kuchelewa kwa Tanki la Maji na alifika na kuhakikisha huduma hiyo inafika Uvinza Kigoma.
Kufuatia hatua hiyo, Waziri Aweso amefanya maamuzi ya kumuondoa Mkandarasi wa Mradi wa Maji Kazuramimba unaotekelezwa kwa Ufadhili wa Enabel na Mkandarasi akiitwa Nangai Engineering Company Limited baada ya kutembezwa umbali mrefu bila kuona vituo vya Maji akiongozana na wananchi wenye hasira kali.
Wakati wa ziara hiyo, Aweso hakuridhishwa na kasi ya Mkandarasi katika utekelezaji wa mradi huo ambao umeanza toka Novemba, 2020 na alitakiwa kukamilisha kazi katika kipindi cha miezi tisa na badala yake sasa ni mwaka wa tatu.
Hata hivyo, Awezo pia amemundoa kufanya kazi hiyo, kuivunja kamati ya Maji ya Mradi huo na kuitaka RUWASA kukamilisha mradi huo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na kuusimamia.