Mke wa Rais wa Marekani, Donald Trump, Melania Trump, ametoa shinikizo la kutaka kufukuzwa kazi kwa mshauri msaidizi wa masuala ya Usalama nchini Marekani, Mira Ricardel mtu ambaye Maafisa wa Ikulu wanasema hajawahi kukutana naye.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Melania, Stephanie GrishamIt imesema kuwa Mshauri huyo amepoteza hadhi ya kuihudumia Ikulu ya nchi hiyo.
Aidha, inasemekana kuwa siku za hivi karibuni, Ricardel amewahi kuzozana na Wafanyakazi wa Melania kwenye ndege katika safari yake ya Barani Africa na kusambaza taarifa za uongo kuhusu tukio hilo, kitu ambacho kimekanushwa na Afisa mkubwa wa Ikulu.
“Ricardel hajawahi kukutana na Mke wa Trump na kuwa Mshauri huyo anafanya kazi kama mmoja wa Wanawake wenye vyeo vikubwa kwenye utawala,”amesema Afisa huyo wa ngazi ya juu Ikulu
-
Waziri ajiuzulu baada ya kuanikwa mitandaoni akijichua
-
Mwanamke aliyejioa nchini Uganda atimiza malengo yake
-
Gutteres azitaka Israel na Hamas kusitisha mapigano
Hata hivyo, Jumanne mchana Novemba 13 mwaka huu, Mamlaka zilisema kuwa Mshauri huyo msaidizi wa Masuala ya Usalama hajafukuzwa kazi na bado anafanya kazi katika Ikulu ya Marekani.