Kiungo Jonas Mkude ameanza mazoezi mepesi chini ya Daktari wa viungo, Jallow Bakari kutokana na jeraha lake la mguu kuendelea kupona taratibu.
Mkude alipata jeraha hilo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC uliopigwa katika Uwanja wa Mo Simba Arena wiki iliyopita ambao ulimalizika kwa ushindi wa mabao 3-1.
Kwa mujibu wa daktari, Mkude hakuwa amepata jeraha kubwa kama ilivyodhaniwa na wengi na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili ili kupona kabisa.
Mkude aligongana na mlinzi wa kulia wa KMC, Kelvin Kijiri dakika ya 52 ambapo alishindwa kuendelea na mchezo kabla ya kukimbizwa hospitali.
Katika kipindi hiki ambacho timu itamkosa Mkude, eneo la kiungo wa ulinzi litakuwa chini ya Mzamiru Yassin, Gerson Fraga na Said Ndemla.