Inaelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Young Africans, Luc Eymael ameonyesha nia ya kutaka kuwa na mshambuliaji wake namba moja David Molinga msimu ujao,akiwa ametupia mabao nane.

Molinga alileta utata Juni 10 kwa kueleza kuwa anachukiwa na viongozi jambo lililoofanya wamuache kwenye safari ya Shinyanga mwisho wa siku viongozi walikana na kumsafrisha kwa ndege pamoja na kocha.

Chanzo kutoka ndani ya uongozi wa Young Africans kimesema kuwa, Eymael aliuambia uongozi kwamba anahitaji kuwa na Molinga kwa msimu mmoja zaidi kwa kuwa anaamini nyota huyo anaweza kuwa msaada msimu ujao katika eneo la ushambuliaji.

“Tulikuwa na kikao na kocha baada ya yeye kuwasili nchini akitokea Ubelgiji, tulizungumza mambo mengi ikiwemo sababu za Molinga kugoma kuondoka na timu, baada ya kumaliza suala la Molinga, ndipo aliomba mchezaji huyo aongezewe mkataba akiamini anaweza akafanya vizuri msimu ujao,” kilisema chanzo hicho. 

Mkurugenzi wa Mashindano na Kaimu Katibu Mkuu wa Young Africans, Thabit Kandoro ambapo alisema: “Tulikuwa na kikao na mwalimu ndiyo na tulizungumza mambo mengi ikiwemo ishu ya Molinga kugoma kusafiri na timu, ila hayo ya kumuongezea mkataba siyajui.”

Chanzo:Championi

Mkude anarudi mdogo mdogo
Callum Hudson-Odoi akwepa kifungo