Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo leo Machi 30, 2021 amethibitisha kuwa wanamshikilia kwa mahojiano Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Tanzania (TPA) Deusdedit Kakoko aliyesimamishwa kazi na Rais Samia Suluhu Hassan.
Mhandisi Kakoko, alisimamishwa kazi machi 28, 2021 ili kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa Tsh. Bilioni 3.6 Bandarini ambao ulitajwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Aidha Brigedia Mbungo amesema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu yanaoendelea kusemwa kuwa walimkamata akiwa anatoroka huku akisisitiza kuwa hatua hiyo ya kushikiliwa ni utaratibu tu wa uchunguzi.
“Hapana sisi hatuna huo ukweli wa kutoroka lakini tumemshikilia kwa sababu ambazo isingekuwa vyema mimi niziongee hapa sasa hivi, lakini ni utaratibu tu wa uchunguzi,” – Brigedia Jenerali John Mbungo.