Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais.

Kwa mujibu wa Sheria, Dkt.Mpango atapigiwa kura na Wabunge wote ambapo atatakiwa kupata kuanzia 50% ya kura ili kuwa Makamu wa Rais.

Jina la Mpango limesomwa bungeni na Spika wa bunge Job Ndugai baada ya kupokea bahasha yenye jina hilo kutoka kwa mpambe wa Rais Samia.

Jina la Dk Mpango liliwekwa katika bahasha mbili ya juu ilikuwa ya kaki na ya ndani ilikuwa nyeupe, Spika Ndugai alianza kusoma nyaraka hiyo ya rais akirudia rudia maneno ya utangulizi kabla ya kulisoma jina.

Makamu wa Rais: Bunge lampitisha Dkt. Mpango kwa 100%, kuapishwa kesho
Mkurugenzi mkuu TPA ashikiliwa kwa uchunguzi