Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeidhinisha jina la Makamu wa Rais Mteule, Dkt. Philip Mpango kwa asilimia 100.

Jina la Dkt. Mpango liliwasilishwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika Bunge hilo leo Machi 30, 2021.

Aidha, taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imeeleza kuwa Makamu wa Rais Mteule, Dkt. Mpango ataapishwa kesho, Machi 31, 2021, Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma kuanzia saa tisa alasiri.

Kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 49 inaeleza kuwa Makamu wa Rais ataapishwa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kula kiapo cha uaminifu kinachohusiana na kazi yake.

Uthibitisho wa Bunge unamuondolea Philip Mpango kuwa Mbunge wa Buhigwe kwa mujibu wa kifungu 37 (3) cha sheria ya taifa ya uchaguzi sura 343 ambapo Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai ameitaarifu Tume ya Taifa NEC kuwa jimbo la Buhigwe sasa liko wazi.

Askofu Gwajima: Mama Samia ni Konki Fire
Dkt. Mpango apendekezwa kuwa Makamu wa Rais