Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amesema kuwa vyombo vya Ulinzi na usalama vinakabiliana na matukio ya uhalifu yanayotokea nchini hivyo ana imani matukio hayo yatakwisha.
Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kwa sasa wanataka kujiridhisha kuwa silaha hizo zinazotumika na hao wahalifu zinatoka wapi na watu hao wasiojulikana ni watu wa aina gani.
Mabeyo amewataka wananchi kuviacha vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi yake bila kuingiliwa na taasisi yeyote kwani vinatekeleza nmajukumu yake kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.
“Haya matukio tunaendelea kukabiliana nayo kama yale matukio ya Kibiti, kwanini matukio ya Kibiti hayaleti mshtuko mkubwa sana sasa wakati watu waliothirika ni wengi zaidi kuliko matukio ya sasa? Mimi sitaki kuingia huko lakini nasema vyombo vya ulinzi na usalama wakati wote vinakabiliana na matukio kadili yanavyojitokeza na ninaamini hali itakuwa shwali na sasa vinashughulika, hoja ya msingi tunataka kujiridhisha silaha hizi zinatoka wapi? Hawa watu ni wa aina gani sasa vyombo mviachie vifanye kazi yake msitoa majibu haraka,”amesema Jenerali Mabeyo
-
Jeshi la polisi Mtwara labaini mtandao wizi wa mafuta na vifaa vya ujenzi
-
Kaskazini Pemba yaanza kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. Shein
Hata hivyo, Jenerali Mabeyo amewatoa hofu wananchi kwa kuwataka waendelee na shughuli zao, kwani vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi yake kwa umakini zaidi.