Baada ya kuwepo kwa sintofahamu juu ya Mkuu mpya wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kushika nyadhifa mbili ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, CCM imesema suala hilo litaamuliwa na Kamati Kuu ya chama hicho.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa kila kitu kipo kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho hivyo suala la mkuu huyo wa mkoa kuwa na kofia mbili litaamuliwa kwenye mkutano wa kamati kuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
”Kanuni ya uchaguzi ya CCM inaeleza bayana mtu mmoja kofia moja, lakini pia kanuni imetoa mamlaka kwa kamati kuu ya chama kumwezesha mtu mmoja kushika kofia mbili endapo itaona inafaa na kamati chini ya Mwenyekiti Ndugu Magufuli itakaa hivi karibuni na itaamua kama aendelee na kofia zote au moja,”amesema Polepole.
-
Video: Fedha za ruzuku za Chadema hutafunwa na akina Mbowe, Lema na Mdee- Msukuma
-
Fredy Lowassa kurithi mikoba ya baba yake Monduli
-
Kalanga aivuruga CCM Monduli, wengine wakimbilia Chadema
Hata hivyo, Chalamila aliteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli pamoja na viongozi wengine wa mikoa na wilaya ambapo jana kupitia mkutano wake na viongozi wa dini mkoa wa Mbeya aliweka wazi kuwa hawezi kujiuzulu uenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa labda apokee maelekezo kutoka kwa Rais ambaye amemteua.