Takriban watu 17 walijeruhiwa katika mlipuko wa bomu, uliotokea katika soko la Macampagne huko Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mkuu wa Wilaya ya blue-collar, amesema kuwa majeruhi katika tukio hilo walipelekwa kwenye vituo vya vya afya kwaajili ya kupatiwa matibabu.

Eneo la Beni ni mojawapo ya maeneo yenye hali tete mashariki mwa DRC, ambayo yamekuwa yakikumbwa na ukosefu wa usalama kwa takriban miaka 30.

Mnamo Januari 15, shambulio lililolaumiwa kwa Allied Democratic Forces (ADF), kundi lenye mfungamano na wanajihadi wa kundi la Islamic State, liliua takriban watu 15 katika kanisa la kiinjili la Kiprotestanti huko Kasindi, kwenye mpaka na Uganda.

Kwa mujibu wa AFP, “Kijana mmoja aliacha begi la kijani kibichi…akiahidi kurejea na kulichukua. Dakika tatu baadaye, begi hilo lililipuka na kuwajeruhi watu nikiwemo mimi na wateja waliokuja kusaga mihogo,” Dany Siauswa, aliiambia AFP.

Wanamgambo hao, wanatuhumiwa kuwaua wanakijiji wasiopungua 23 siku ya Jumatatu. Shambulio hilo lilidaiwa na kundi la Islamic State na operesheni ya pamoja ya jeshi la Kongo na Uganda inayolenga ADF katika eneo hilo imekuwa ikiendelea tangu mwishoni mwa 2021.

Gharama za upandikizaji mimba kupunguzwa
Afrika ni lazima ijifunze kujilisha: Senegal