Shule 29 za msingi na awali katika Manispaa ya Ubungo zimefungiwa kwa kukosa usajili baada ya ukaguzi unaoendelea wa kukagua shule zote katika Manispaa hiyo, ukaguzi ambao unalengo la kuhakikisha elimu inayotolewa ni ile inayokidhi vigezo.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Manispaa ya Ubungo, Bornwell Kapinga ambapo amesema kuwa zoezi hilo lilianza juzi na kuwa baada ya kubaini shule hizo hazina usajili walizifungia hadi hapo zitakapofuata taratibu za kusajili.
“Ukaguzi huu ulifanywa kwa kushirikiana na Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Ubungo, Chausiku Masegenya ambapo waliwaagiza wamiliki shule hizo kufuata taratibu za usajili na endapo hamtafanya hivyo wahamisheni wanafunzi na muwapeleka katika shule nyingine. Natoa wito kwa wamiliki wote wa shule mfuate taratibu pindi mnapotaka kuwekeza kwenye elimu kwani ubora wa elimu unaanzia katika usajili,”amesema Kapinga
-
Lissu aungwa mkono na Kituo cha Haki za Binadamu LHRC
-
Kamanda Mambosasa: Kila mtu ni mtekwaji mtarajiwa
Aidha, amesema kuwa lengo la kufanya ukaguzi huo ni kuboresha elimu katika Manispaa hiyo lakini pia kudhibiti utitiri wa shule lukuki ambazo zimekuwa zikifunguliwa kiholela katika Manispaa hiyo ambazo pia hazina ubora unaotakiwa.
Hata hivyo, Manispaa ya Ubungo ina jumla ya shule za msingi zilizosajiliwa zipatazo 127 ambapo shule 63 ni shule binafsi na shule 64 ni za serikali