Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA John Mnyika amesema chama hicho bado kinatamani kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, na kuwa wanachosubiri ni ofisi ya Ikulu kuwajibu juu ya tarehe ya Rais kukutana na chama hicho.
Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuna mambo mengi yaliyojitokeza ukiachilia mbali masuala ya uchaguzi 2020 ambayo yanahitaji mazungumzo.
“Ni muhimu tukaeeleza wazi milango yetu sisi CHADEMA kukutana na rais bado ipo wazi tunachosubiri ni Ikulu kuweza kututaarifu kama Rais yupo tayari kukutana vyama vya siasa kama alivyoahidi na Chadema tupo tayari,” amesema Mnyika.
“Kuna mambo yaliyojitokeza na uchaguzi 2020 sasa yamejitokeza mambo mengine zaidi yenye uharaka wa mazungumzo sisi kama Chadema hatujafunga milango ya makutano na rais” amesema Mnyika
“Katiba mpya imekuwa kilio cha wananchi kwa muda mrefu kuna ushahidi wa moja kwa moja wakati wa mchakato wa Katiba tume ya mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Warioba ilivyozunguka na kukusanya maoni ya wananchi, wananchi walisema wanataka Katiba mpya na Katiba ya iana gani?” amesema Mnyika.