Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC Mohamed Dewji amerejea kwenye nafasi ya Uenyekiti baada ya jana kutangaza kujiengua kufuatia kipigo cha 1-0 kwenye fainali ya MapinduziCup2020 dhidi ya Mtibwa.
MO Dewji jana alifikia maamuzi mazito ya kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti na kubakia kama muwekezaji wa Simba.
MO alifikia hatua hiyo kutokana na timu hiyo kutofanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakitolewa na UD Songo ya Msumbiji hatua ya awali, sare ya 2-2 dhidi ya Yanga inayoonekana kupitia kipindi kigumu kiuchumi na kupoteza fainali ya leo ya Mapinduzi Cup 1-0 dhidi ya Mtibwa.
“Kilichotokea kwenye akaunti zangu jana kilikuwa ni bahati mbaya, tuko pamoja, tunarudi kwenye ligi tukiwa na nguvu , tunajipanga kwa ajili ya ligi, nawapongeza Mtibwa kwa kuchukua kombe, mimi ni Simba damudamu, nitabaki kuwa Simba” – MO DEWJI