Kabla ya kusajiliwa na Chelsea mshambuliaji wakihispania Alvaro Morata alikuwa akiwindwa na mashetani wekundu Manchester United ambao baadae waliamua kumsajili Romelu Lukaku kutoka Everton.
Morata amesema mwanzoni mwa msimu wa usajili hakujua kama Chelsea wanamuhitaji lakini alijua fika kuwa Man Utd walikuwa na nia ya kumsajili na baadae aliposikia anakiwa na Conte hakusita kujiunga na kocha huyo aliyewahi kumfundisha akiwa Juventus.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amesema uwepo wa Conte katika klabu ya Chelsea ndio sababu kubwa iliyomfanya kuitosa Manchester United na kujiunga na Chelsea.
-
Defoe aing’arisha Bournemouth
-
Dunia kushuhudia pambano la mwaka la masumbwi leo, Canelo Vs Triple G
-
Conte aitabiria Arsenal ubingwa
Akiwa kocha wa Juventus Antonio Conte alifanya kazi na Morata mwaka 2014 wakati mchezaji huyo aliposajiliwa akitokea Real Madrid lakini hata hivyo baada ya miezi miwili tu Conte aliachana na Juventus baada ya kuchukua kibarua kipya cha kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Italia.
”Klabu nyingi zilinihitaji sio tu Man Utd na Chelsea na lakini kitu muhimu nilichoongea na Conte ni kwamba alitaka nije hapa”, alisema Morata.
Morata alisajiliwa na Chelsea akitokea Real madrid kwa kiasi cha Pauni milioni 58 na tayari amefunga mabao matatu katika michezo mitatu aliyoichezea Chelasea.