Ikiwa tayari imeshawasajili wachezaji wanne tangu dirisha la usajili lilipofunguliwa Agosti Mosi, tetesi zinaeleza kuwa klabu ya Young Africans huenda ikawatema wachezaji zaidi ya 10, ili kutoa nafasi kwa wachezaji wanaotarajiwa kuleta mabadiliko kuanzia msimu wa 2020/21.

Tetesi hizo zinaeleza kuwa wachezaji watakaoachwa klabuni hapo, wanakabiliwa na sababu kadhaa ikiwemo ya utovu wa nidhamu pamoja na kushuka kwa viwango, huku wengine mikataba yao ikifikia ukingoni.

Wachezjai wanaotajwa huenda wakatemwa na Young Africans ni

1. Benard Morisson➡ Nidhamu mbovu

2. Papy Tshishimbi➡Nidhamu pia mkataba umeisha

3. Kelvin Youndan➡Nidhamu mbovu

4. Japhary Mohamed➡Kiwango duni

5. Raphael Daud➡Kiwango duni

6. David Molinga➡Nidhamu mbovu

7. Ally Ally➡Kiwango duni

8. Ally Mtoni Sonso➡Kiwango duni

9. Andrew Vicent Dante➡Kiwango duni

10. Sospeter➡Kiwango duni

11. Adam Kiondo➡Kiwango duni

12. Tariq Seifu Kiakala➡Kiwango duni

13. Juma Mahadhi➡Kiwango duni

14. Paul Geofrey Boxer➡Kiwango duni

15. Foruck Shikalo➡Kiwango duni

16. Yikpe➡Kiwango duni

17. Erick Kabamba➡Kiwango duni

18. Adeyum Saleh➡Kiwango duni

19. Gustavo Simon➡Kiwango duni

20. Mohamed Banka➡Nidhamu pia mkataba umeisha

Wachezaji waliosajiliwa na Young Africans hadi sasa ni Mshambuliaji Waziri Junior Shentembo akitokea Mbao FC walioporomoja Daraja, kwa kufungwa na IHEFU FC kwenye mchezo wa mtoano, mwishoni mwa juma lililopita.

Zawad Mauya kutoka Kagera Sugar, Bakari Mwamnyeto kutoka Coastal Union na Yassini  Mustapha wa Polisi Tanzania FC.

Fedha za FIFA kunufaisha mikoa Tanzania Bara, Zanzibar
Makonda'' nimekamilisha safari yangu ya ukuu wa mkoa''