Mshambuliaji kutoka nchini Zambia na Klabu ya Simba SC Moses Phiri ana matumaini ya kuwa sehemu ya kikosi kitakachoelekea Guinea kwa ajili ya mchezo kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya Makundi.

Simba SC itaanza kupambana dhidi ya Horoya AC katika mchezo wa Kundi B, lenye timu nyingine za Raja Casablanca (Morocco) na Vipers SC (Uganda).

Mshambuliaji huyo ambaye aliumia wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar mwishoni mwa mwaka 2022, amesema kwa kasi anayoenda nayo baada ya kuanza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake, ana matumaini makubwa ya kuwa sehemu ya safari ya Guinea.

Phiri amesema amekua na Program maalum chini ya uangalizi wa Madktari wa Simba SC, ambazo anaamini zinamuwezesha kurudi kwa kasi katika hali yake ya kawaida.

“Ninashukuru nimefanikiwa kupona kwa kiasi kikubwa na kuanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzangu kwa ajili ya michezo inayotukabili kwa siku za karibuni, licha ya kuendelea kubaki chini ya uangalizi wa madaktari.”

“Ninaamini kwa kasi ya Program ambazo ninaendelea nazo kwa sasa, nitakuwa tayari kucheza kabla ya mchezo wetu wa kwanza Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.” amesema Phiri

Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 10 katika Ligi Kuu Tanzania Bara, alikua na mchango mkubwa kwenye michezo ya hatua za awali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu, akifunga mabao matano katika michezo minne.

Katika ushindi 2-0 wa Simba SC dhidi ya Nyasa Big Bullet ya Malawi, Phiri alifunga ugenini mjini Lilongwe, kabla ya kufanya hiyo katika mchezo wa nyumbani Dar es salaam alifunga mabao mawili ya ushindi.

Mchezo dhidi ya 1º de Agosto ya Angola, Phiri alikuwa miongoni mwa wachezaji walioipa ushindi Simba SC ugenini wa 3-1, kabla ya kufanya hivyo tena kwenye mchezo wa nyumbani Dar es salaam.

Simba SC itacheza dhidi ya Horoya AC mjini Conakry, katika Uwanja wa General Lansana Conté, Febriari 11 majira ya saa kumi jioni kwa saa za Guinea.

Ruto Vs Kenyatta: IGP aeleza sababu za kumpunguzia Uhuru Kenyatta walinzi
Beki US Monastir amuhofia Fiston Mayele