Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na Klabu ya Real Madrid Karim Benzema anatarajiwa kuwa FIT kwa ajili ya mchezo wa Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Liverpool mapema mwezi Machi.

Mshindi huyo wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia ‘Ballon d’Or holder’ alipata majeraha ya paja usiku wa kuamkia leo, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Valencia iliyokubali kufungwa 2-0.

Maneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti alionesha kuwa na wasiwasi na jeraha ya Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35, lakini baadae alithibitisha Benzema atakuwa sawa kabla ya mchezo dhidi ya Liverpool.

Kwa mantiki hiyo Benzema hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Real Mallorca keshokutwa Jumapili (Februari 05), na kisha Michuano ya Klabu Bingwa Duniani inayoendelea nchini Morocco.

Kwenye Michuano hiyo Real Madrid itaanzia hatua ya Nusu Fainali, ikimsubiri mshindi kati ya Al Ahly (Africa) dhidi ya Seattle Sounders FC (Amerika ya Kati na Kaskazini) zitakazokutana kesho Jumamosi (Januari 04).

Lissu: Siuwazi urais wa Tanzania
Azam FC yaifuata Dodoma Jiji FC