Takriban watu wasiopungua 13 wamefariki kwa ajali ya moto uliozuka alfajiri katika Hosteli moja iliyopo mji mkubwa zaidi wa Kazakhstan, Almaty ambayo ilikuwa na watu 72 waliokuwa wakiishi ndani ya jengo hilo huku 52 kati yao wakihamishwa salama.

Moto huo, ulianza katika ghorofa ya chini ya jengo hilo la ghorofa tatu, ambalo liligeuzwa kuwa hosteli wiki kadhaa zilizopita, bila ya kufanyiwa ukarabati kutokana na hali yake.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa vifo hivyo vilitokea baada ya waathiriwa kukosa hewa katika ghorofa ya chini ya jengo hilo, huku maafisa wakianza uchunguzi ju ya tukio hilo.

Idara ya hali ya dharura ya jiji la Almaty imesema, “Moto huo ulizuka katikati mwa mji huo mkuu wa zamani majira ya saa 11:30 Alfajiri. Watu 13 waliokufa wamegunduliwa, na utambulisho wao utabainishwa.”

Ali Maaloul: Tunafahamu ubora na udhaifu wao
Benchikha abeba matumaini, timu ikienda Botswana