Takribani watu 23 wamekufa kwa kipindupindu katika jamii zilizohamishwa na mafuriko hivi karibuni mashariki mwa Nchi ya Ethiopia.

Kwa mujibu wa Shirika la Save the Children zaidi ya wagonjwa wa Kipindupindu wamethibitishwa katika muda wa wiki mbili pekee katika eneo la Somalia, eneo lililoathiriwa zaidi na mafuriko ya hivi karibuni na mvua kubwa isiyo ya kawaida.

Mvua hiyo, imewaathiri watu milioni 1.5 kote nchini huku idadi ya watu waliolazimika kuacha makazi yao ikifikia 600,000, UN ilisema.

Hata hivyo, ni asilimia 10 tu ya walioathirika kwa sasa wanapokea misaada huku Ethiopia ikiendelea kukabiliwa na mapungufu katika ufadhili, iliongeza.

Zaidi ya Wilaya 90 nchini Ethiopia, zimeripoti matukio ya ugonjwa wa kipindupindu huku shirika la Save the Children likionya kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwani mvua nyingi zinatarajiwa kunyesha katika takribani mikoa mitatu.

Mvua kubwa iliyonyesha Ethiopia, pamoja na Somalia na Kenya, imesababishwa na hali ya hewa ya El Niño pamoja na nyingine inayojulikana kama Dipole ya Bahari ya Hindi.

Ugomvi wa uke wenza wasababisha uharibifu wa mali
Benchikha: Ninawajenga wachezaji kisaikolojia