Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amemuaga rasmi Wayne Rooney ambaye ameamua kurejea katika klabu yake ya zamani ya Everton.
Rooney anarejea Everton ikiwa ni miaka 13 baada ya kuihama klabu hiyo na kujiunga na wekundu wa Old Trafford.
“Sio siri kwamba nilikuwa nahamasishwa na Wayne; alikuwa mchezaji wa kuigwa katika kipindi chote akiwa ndani ya klabu na atabaki kwenye historia ya vitabu kwa miaka mingi ijayo,” tovuti ya Manchester United inamkariri Mourinho.
“Sio rahisi kumuona mchezaji mkubwa akicheza soka katika kiwango cha chini tofauti na ambavyo angependa iwe na nisingeweza kuzuia njia alipoomba kurejea Everton. Ujuzi na uzoefu wake pamoja na kujitambua vitakumbukwa daima na namtakia kila la kheri kwa siku za usoni,” ameongeza.
Jumamosi hii, Rooney aliwasili katika viwanja vya mazoezi vya klabu ya Everton, Finch Park kwa ajii ya kufanyiwa vipimo.
Safari ya soka ya Rooney ilianzia katika viwanja vya Goodison Park vya Everton kabla ya kujiunga na Manchester United mwezi Agosti mwaka 2004 kwa dau la pauni milioni 27 ambako alifanikiwa na kupewa nafasi ya unahodha wa timu hiyo.
Dakika chache zilizopita, Rooney ametumia mtandao wa Twitter kueleza jinsi alivyo na hamasa ya kurejea Everton.
Excited to be back at @Everton. Can’t wait to meet up with @RonaldKoeman and the lads! #EFC ? pic.twitter.com/0CjD0i1aXg
— Wayne Rooney (@WayneRooney) July 9, 2017