Mbunge wa Mikumi, ambaye pia ni msanii wa Hip Hop, Joseph Haule (Profesa Jay) amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Grace Mgonjo katika Kanisa la Mtakatifu Joseph lililopo Oysterbay jijini Dar es salaam.

Wapendanao hao wamefunga ndoa Jumamosi Julai ya 08, 2017 kisha amsha amsha ya sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo mamia ya watu walihudhuria sherehe hiyo na kupata nafasi ya kula, kunywa hadi kusaza huku shughuli nzima ikipambwa na mahudhurio ya wanasiasa, mastaa kibao wa Bongo.

Prof. Jay aliingia ukumbini akimuimbia mke wake hali iliyosababisha ukumbi mzima kuzizima kwa shangwe na wote waliungana nao kwa kucheza na kufurahia tukio hilo. Tazama hapa Video

Mourinho atoa maneno ya busara kumuaga Rooney
WBO wakubali kuchunguza na kutoa alama mpya pambano la Pacquiao na Horn