Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi nchini Marekani wanaanza leo kuvijadili vifungu vya sheria vya kumshitaki Rais Donald Trump.
Wanachama pinzani cha democrat wanamtuhumu rais kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuishawishi Ukraine kumchunguza mpinzani wake wa kisiasa, Joe Biden, na kuzuia msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Pia anadaiwa kuzuia uchunguzi wa Bunge kuhusu suala hilo.
Huku wanachama tawala charepublican wanapinga vifungu hivyo vyote vya sheria vya mashitaka dhidi ya rais, wakisema hakufanya kitu chochote kibaya katika mawasiliano yake na Ukraine.
Trump anawatuhumu Wademocrat kwa kujaribu kuyabatilisha matokeo ya uchaguzi wa 2016 ambao alishinda.
Ikumbukwe kuwa baraza la Seneti litahitaji wingi wa theluthi mbili kumuondoa rais madarakani, hatua ambayo siyo rahisi kufanyika. Hii itakuwa ni mara ya tatu tu kwa rais wa Marekani kushitakiwa.