Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina ameagiza kukamilishwa kwa ujenzi wa chanzo cha maji kilichopo katika kijiji cha Igobe Wilayani Meatu ifikapo mwisho wa Mwezi huu.

Mpina, ameagiza kufanyiwa kazi kwa kasoro zilizojitokeza katika mradi huo wenye uwezo wa kuhudumia takribani watu elfu nane katika kijiji cha Mwandoya na Igobe ili kumuwezesha mkandarasi kukamilisha kazi hiyo wa wakati.

“ Lazima Pawepo na usimamizi madhubuti katika mradi huu ili wakazi wa maeneo jirani na mradi, mbali na hapa waweze kunufaika na kama kutajitokeza kwa uzembe wowote wahusika watawajibika kwa mamlaka.” Amesema Mpina.

Aidha, katika ziara yake ya kukagua miradi ya mazingira,  Mpina pia alitembelea shule ya Sekondari ya Mwandoya na kusikiliza kero mbalimbali zilizopo shuleni hapo na kuahidi kushirikiana na uongozi kuweeza kuzitatua.

Hata hivyo, katika ziara hiyo, pia amekagua ujenzi wa wodi mpya ya wazazi inayojengwa katika Zahanati ya Mwandoya kujionea maendeleo ya ujenzi huo ambao unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

 

Video: Bodi ya Korosho yatoa onyo kali kuhusu pembejeo
Kilichomkuta mchungaji aliyefumaniwa na mke wa mtu