Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amepokea Jumla ya Kompyuta za kisasa 100 zenye thamani ya Shillingi Million 210 kutoka kiwanda cha utengenezaji wa nguo zitokanazo na pamba ya Tanzania cha NIDA Textile Ltd.
 
Amesema kuwa Computer hizo atazigawa kwenye vituo vya Polisi 20 kwaajili ya kufungwa mfumo wa kisasa wa kuripoti taarifa za uhalifu zilizoripotiwa kwenye vituo vya Polisi kila siku (Crime Statistic Management Information System).
 
Aidha mfumo utasaidia viongozi kupata taarifa za uhalifu zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi kwa wakati na kupunguza uhalifu kwani taarifa zote za wahalifu zitaonekana kuanzia ngazi ya Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Mkoa, Wilaya na Mkuu wa kituo hivyo kusaidia viongozi kufanya maamuzi.
 
“Tunaachana na kuandika taarifa kwenye makaratasi na makaunta au madaftari kwenye Vituo vya Polisi ambayo baada ya muda mfupi yanapotea na kumuacha Mwananchi hajui kesi yake imeishia wapi, huu mfumo ni ukombozi na mwonekano mpya wa Jeshi la Polisi na hata Wananchi wataachana na matatizo ya rushwa na watu kubambikiziwa kesi” Amesema Makonda.
 
Hata hivyo, Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA, Mohamed Hamza amesema kampuni yao imeamua kuunga mkono jitihada za mkuu huyo wa mkoa katika dhamira yake ya kufanya Mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa Jeshi jijini Dar es Salaam

Video: Agizo la JPM lakwamishwa, Serikali yatikisa benki
Mkojo wa Masogange watetewa kama wa Wema, yadaiwa una ‘Unga’