Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amewataka wakazi wa Mkoa wa Morogoro kutunza Vyanzo vya Maji na Mazingira kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameokoa maisha ya binadamu na viumbe hai.
 
Ameyasema hayo mapema hii leo Mjini Morogoro alipokuwa katika zoezi la usafi kitaifa, amesema kuwa kama wakitunza Mazingira watakuwa wamesaidia wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam Pamoja na Pwani ambao vyanzo vyao vingi vya maji vimetokea katika mkoa huo.
 
“Kutakuwa na ufuatiliaji wa hali ya juu katika utekelezaji wa zoezi la upandaji miti kwa kila wilaya hivyo wananchi mnashauriwa kutunza vyanzo vya maji na kupanda miti,”amesema Mpina.
 
Aidha, Mpina ameunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika suala zima la utunzaji na usafi wa mazingira.
 
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kebwe Steven Kebwe amesema kuwa hali ya mazingira ya mkoa huo ni nzuri na wana mikakati maalumu ya kupambana na uharibifu wa mazingira.
 
Hata hivyo, usafi huo wa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan la kufanya usafi wa Mazingira

Anthony Joshua Ampa Kichapo Klitschko
Hatma ya Chadema 'EALA' kujulikana mwezi ujao