Hatimaye bondia Anthony Joshua leo amekata mzizi wa fitina baada ya kumpiga kwa ‘knock out’ bondia mzoefu na bingwa wa zamani wa dunia wa masumbwi wa uzito wa juu, Wladimir Klitschko, hivyo kuendelea kushikilia mkanda huo.

Joshua alifanikiwa kumaliza pambano hilo katika raundi ya kumi na moja (11) baada ya kumpiga makonde mfululizo bila majibu Klitschko ikiwa ni baada ya kumuangusha chini mara mbili katika raundi hiyo.

Pambano hilo la kihistoria lililofanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Wembley chini Uingereza lilikuwa kali na kufanya mashabiki washindwe kutabiri mshindi hadi ilipofika raundi ya 11.

Joshua alikuwa wa kwanza kumuangusha chini kwa masumbwi Klitchko katika raundi ya tano, lakini Klitschko alijibu katika raundi ya sita kwa kumuangusha chini kwa sumbwi zito.

Ushindi huo unamfanya Joshua mwenye umri wa miaka 27 kuendelea kuweka rekodi ya kushinda michezo yote 19 kwa knockout.

Akizungumza baada ya ushindi huo, Joshua alieleza kuwa ana mheshimu sana Klitschko na kwamba alichokuwa anakifanya ni kujaribu kwa kuwa yeye sio mkamilifu.

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 30, 2017
Mpina atoa neno kwa wakazi wa Morogoro