Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amepokea Shukrani kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan baada ya huduma ya Maji kuwafikia eneo la mpaka kati ya Tanzania na Uganda, eneo lililopo Wilayani Kyerwa, Mkoani Kagera

Aidha, Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng. Nadhifa Kemikimba kusimamia na kuhakikisha upanuzi wa mradi Murongo kwenda Mabale sambamba na kuhakikisha mzabuni kuleta pampu za mradi wa Maji Nyamiaga-Nyakatera, ili ifikapo mwezi wa tisa mradi uwe umetoa huduma ya maji kwa wananchi.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa jimbo la Kyerwa, Innocent Bilakwate amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Kyerwa miradi mingi ya maji yenye thamani ya Bilioni 12 katika kuhakikisha wananchi wa Kyerwa wanafikiwa na huduma ya Maji.

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso pia amezindua mradi wa maji Murongo wenye Gharama ya shilingi 589,317,484.69 na madi huo utahudumia wananchi 6500 waishio katika kijiji cha Murongo.

Wawili washinda Tuzo Uandishi mahiri Habari za ushirika
Mkaguzi chakula cha Rais afichua jambo