Ziwa Victoria sasa litakuwa chanzo cha maji kwa Vijiji 33 vya Wilaya ya Bunda Mkoani Mara na kufanya upatikanaji wa huduma ya Maji kuwa wa uhakika katika maeno hayo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati akiwa katika Ziara ya kikazi Wilayani Bunda alipotembelea mradi wa Maji unaotekelezwa kwa kutumia chanzo cha ziwa Victoria Kijijini Tiring’ati.
Amesema, tayari Mtaalam Mshauri amekamilisha usanifu wake na Serikali ina mpango wa kutoa maji kutoka Tanki la Maji Butiama lenye ukubwa wa lita milioni 2.5, katika Mradi wa Maji Safi Mugango -Kiabakari, kupeleka Nyamuswa kupitia Bisarye.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini, Boniface Getere ameishukru Serikali kwa uamuzi wa kutumia chanzo cha Maji cha uhakika cha Ziwa Victoria, ili kuboresha huduma ya maji kwenye Wilaya ya Bunda.