Mshambuliaji Kikosi cha Simba Queens Oppa Clement amesema hadi sasa hajasikia lolote kuhusu kutakiwa na baadhi ya vilabu vya Soka huko Barani Ulaya, ambavyo vimeripotiwa kuvutiwa na uchezaji wake.

Oppa amesema huenda taarifa za yeye kuhitajika barani Ulaya zimeufikia uongozi wake, lakini kwake kama mchezaji hana taarifa hizo na badala yake amejipanga kuisaidia Simba Queens kwenye mchezo wake wa kesho dhidi ya Mamelodi Sundowns Ladies.

“Sijasikia taarifa zozote za kuwaniwa na klabu za Barani Ulaya, labda upande wa Uongozi huenda ukawa na taarifa zaidi, kwa sasa nimejikita katika mpango wa kuisaidia timu yangu kwenye mchezo wa Nusu Fainali ambao tutacheza baadae leo Jumatano dhidi ya Mamelodi Sondowns Ladies.”

“Ikitokea kweli na ikathibitishwa nina imani Uongozi wa Simba SC utanikubalia kuondoka kwa sababu hauna tabia ya kuwakatalia wachezaji wake pindi inapotokea nafasi ya kwenda kucheza soka nje ya nchi.” amesema Oppa

Oppa Clement aliwahi kwenda kufanya majaribio nchini Uturuki mapema mwaka huu, lakini hakufanikiwa kusajiliwa nchini humo na badala yake alirejea Simba Queens na kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara pamoja na ile Kanda ya Afrika mashariki na kati CECAFA.

George Mpole: Sitamani kurudi Geita Gold FC
Oppa Clement atajwa kikosi bora Afrika