Mshambuliaji wa Tanzania na Simba Queens, Oppa Clement ametajwa kwenye Kikosi Bora Cha Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa Wanawake, inayoendelea nchini Morocco.

Orodha ya wachezaji 11 imetangazwa kwenye Mitandao ya kijamii ya Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF, huku jina la Mshambuliaji huyo likionekana katika safu ya Ushambuliaji.

Orodha hiyo imetajwa baada ya kufanywa kwa tathmini ya kina na ya kiufundi kwa michezo ya hatua ya Makundi ya Michuano hiyo iliyofikia tamati mwishoni mwa juma lililopita.

Oppa meonesha uwezo mkubwa kwenye Michuano hiyo, akiisaidia Simba Queens kufika hatua ya Nusu Fainali, huku akifunga mabao mawili kwenye Michezo mitatu.

Mshambuliaji Simba Queens awaniwa Ulaya
Simulizi ya Majaliwa alivyowaokoa watu 24 ajali ya Ndege