Mshauri wa zamani wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Fortunat Biselele ambaye aliondolewa katika Baraza la Mawaziri wiki iliyopita (Januari 14, 2023), bila ya kutolewa sababu, amepelekwa gereza kuu jijini Kinshasa.

Biselele ambaye ni mshauri aliyekuwa na ushawishi mkubwa kwa Rais Felix Tshisekedi, alihamishiwa kwenye gereza kuu la Makala jana usiku (Januari 20, 2023), baada ya kesi yake kusikilizwa kwa saa sita.

Fortunat Biselele akiwa chini ya ulinzi mkali. Picha ya Mediacongo.net

Vyanzo mbalimbali vya Habari, vinadai kuwa Biselele anashukiwa kushirikiana na Serikali ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame kuihujumu DRC, akijaribu kuileta Kinshasa karibu zaidi na Kigali mwanzoni mwa utawala wa Tshisekedi.

Hata hivyo, mapema mwishoni mwa juma, Rwanda iliishutumu Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo – DRC kwa kuyapuuza makubaliano yanayolenga kuleta amani katika eneo la mashariki la nchi hiyo linalokabiliwa na mgogoro.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 22, 2023
Dodoma Jiji FC yaitambia Simba SC