Rekodi ya kulala chini ya saa 117, iliwekwa kwenye shindano la mwaka jana (2022), katika Kijiji cha mapumziko cha Donja Brezna, lakini mashindano ya mwaka huu 2023 yameingia siku ya 22 hii leo Septemba 9, 2023 ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha zawadi ya Shilingi Milioni 2.6.
Mratibu na Mmiliki wa Hoteli hiyo, Radonja Blagojevic amesema shindano hilo lilizinduliwa katika nchi ndogo ya Adriatic miaka 12 iliyopita, ili kudhihaki hadithi maarufu inayowataja Wamontenegro kuwa ni wavivu kupindukia, alisema.
Washindani hao kwa nyakati tofauti wamesema, “Sote tunajisikia vizuri, bora, hakuna shida za kiafya, wanatubembeleza, tunachopaswa kufanya ni kubaki chini, na tunafurahia uwepo wa bingwa wa mwaka 2021 Dubravka Aksic (38).”
Amesema, washiriki saba waliosalia kutoka uwanjani wa kuanzia 21 walikuwa wamelala chini kwa saa 463 hadi sasa na Watu wa nchini Uingereza wao walijiorodheshwa wakiwa na kampeni ya kuwaelimisha kuwa kufanya kazi kwa bidii kungewaleta maisha bora.
Hata hivyo, sheria za shindano hilo zinawaelekeza kuwa, kitendo cha kusimama au kuketi ni ukiukaji na sababu za kutohitimu, lakini washiriki wanaruhusiwa kuwa na dakika 10 kila baada ya saa nane za kwenda msalani na wanaruhusiwa kutumia simu za mkononi au laptops.