Beki wa kati Ibrahim Ame amefunguka, baada ya uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC kumpa ruhusa ya kutafuta changamoto mpya kwenye timu nyingine.

Ame alisajiliwa Simba SC mwishoni mwa msimu wa 2019/20, akitokea Coastal Union ya Tanga, lakini ameshindwa kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Beki huyo anatajwa kuwa kwenye mipango ya kusajiliwa na Mtibwa Sugar au Kagera Sugar kwa mkopo akitokea Simba SC, ili kulinda kipaji chake na pengine kuongeza juhudu ambazo zitamshawishi kocha Gomes, kumrudisha kundini mwishoni mwa msimu huu.

Tayari amethibitisha kuwa mbioni kujiunga na klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kusema: “Nimepewa nafasi ya kusaka timu ya kunipa changamoto msimu ujao baada ya kukaa benchi muda mrefu na tayari nipo kwenye mazungumzo na hizo timu.”

“Biashara United Mara pia walionyesha nia lakini dau lao halijaniridhisha hivyo ninachoweza kukwambia nitakuwa mchezaji wa walima miwa.” amesema Ame.

Amesema mbali na kutaka kudhihirisha hilo pia lengo lake la kwenda kwa mkopo ni kuonekana na kupata nafasi ya kuitwa timu ya taifa huku akifafanua kuwa wachezaji wanaoitwa kikosi cha taifa haoni kama wanamzidi sana kiuwezo isipokuwa wao wanaonekana uwanjani na yeye amekuwa akikaa benchi.

Nabi aomba muda wa kuandaa kikosi chake
Kapombe, Nyoni wapata msamaha kambini