Kocha mkuu wa Young Africans, Nassredine Mohamed Nabi ametua nchini jana Jumanne (Agosti 24) na kutamka kwamba bado hajapata muunganiko katika timu yake licha ya kuwa nchini Morocco kwenye maandalizi ya msimu mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Nabi alisema; “Muunganiko wa timu bado, tunahitaji muda kama mwezi au miezi mitatu kwa sababu timu haijengwi kwa muda mfupi.”

“Wachezaji wote tuliowasajili ni wazuri kwa sababu tulikuwa tunawafuatilia, tukipata muda zaidi tutakuwa bora zaidi,” alisema Nabi.
Naye mshambuliaji Saido Ntibazonkiza alisema; “Kama kocha alivyosema muda ulikuwa mchache lakini tukiunganika vizuri tutakuwa bora zaidi, kikosi kipo vizuri.”

Young Africans waliweka kambi ya juma moja nchini Morocco kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika 2020/21.

Wakati huo huo Kikosi cha Young Africans kitatambulishwa rasmi Jumapili (Agosti 29) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kwenye kilele cha Wiki ya Mwnaanchi (Siku ya Mwananchi).

Siku hiyo Young Africans yenye wachezaji wapya kwa asilimia kubwa itaonekana kwa mara ya kwanza ikicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Zanaco FC ya Zambia.

Mkurugenzi Tume ya TEHAMA azindua Tuzo
Mtibwa Sugar, Kagera Sugar zamuwania Ibrahim Ame