Mkurugenzi Tume ya Tehama, Samson Mwela, leo Agosti 25, 2021 amezindua Tuzo za TEHAMA Nchini ambapo tuzo hizo washiriki watapendekezwa na wananchi wanaotumia Teknolojia zinazoendeshwa na makampuni ya Bima, Elimu,Afya na mtu mmoja mmoja.

Mwela amesema zoezi hilo linaanza leo Agosti 25, 2021 ambapo wananchi wenyewe watapendekeza.

“ICT Awards itawapa Watanzania wenyewe nafasi ya kupendekeza majina ya Watu au kampuni za watoaji wa huduma bora wa Tehama nchini, ambapo zoezi limezinduliwa leo Agosti 25, 2021 kwenye tovuti ya tume yaani https://www.ictc.go.tz/ hadi Septemba 10” amesema Mwela

“Baada ya zoezi la kupendeza washiriki kukamilika, Septemba 11-18 waliopendekezwa watajaza fomu Maalum wakieleza nini wamefanya ambacho kilipelekea wakapigiwa kura na Wananchi” amesema Mwela

Wanawake wazuiwa kufanya kazi Afghanistani
Nabi aomba muda wa kuandaa kikosi chake