Pamoja na kupoteza kwa mabao 3-1 kutoka kwa Polisi Tanzania lakini timu ya Mtibwa Sugar imeeleza haijakata tamaa na itapambana kutoshuka daraja kwenye mechi zao mbili zilizosalia.

Kipigo hicho walichokipata juzi Jumatatu (Mei 15) kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi kimeifanya Mtibwa iendelee kubaki na alama 29 kwenye nafasi ya 14 wakipambana kutocheza hatua ya mtoano kuwania kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

Kocha Msaidizi wa Mtibwa, Awadh Juma amekiri ugumu wa ligi msimu huu umechangia wao kuwa na matokeo ya namna hiyo ingawa amesema hilo halijawakatisha tamaa kutafuta matokeo kwenye mechi zao zinazokuja.

Naye Kocha Msaidizi wa Polisi, John Tamba amesema: “Tumemaliza salama, niwapongeze wachezaji wangu walipambana kama vile tulivyowaelekeza na tumepata alama tatu, mchezo haukuwa rahisi, lakini kipindi cha pili vijana tuliwaelekeza udhaifu wa Mtibwa wakafanya kazi na sasa tunatazama michezo ijayo.”

Pamoja na ushindi huo, Polisi imesalia nafasi ya 15 na alama 25 ikiwa imebakiza mechi mbili dhidi ya Simba SC na Azam FC ambazo zote itakuwa ugenini huku Mtibwa ikibakiza miwili nyumbani michezo dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold.

Wawili waongezwa kinyang'anyiro Spurs
Kashfa ya vyandarua yang'oa bodi nzima Kemsa