Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya CUF, Abdallah Mtolea amesema kuwa licha ya kujiuzulu kwenye nafasi yake bado ana mahusiano mazuri na waliokuwa wabunge wenzake wa upinzani na kusisitiza kuwa mahusiano hayo yatazidi kuendelea kuimarika.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa amejipanga vizuri kuhakikisha anawania tena nafasi ya Ubunge kwenye jimbo hilo baada ya kuhama chama.
Amesema kuwa siasa haina udaui na kwamba wabunge wote wa upinzani ni watu ambao amekuwa akishirikiana nao kila siku.
“Mimi sina uadui na Mbunge yeyote, kwa kifupi wabunge wa vyama vyote ni marafiki zangu, kuhusu kama wanahofu kwamba ukaribu wangu nitakuwa nikiwashawishi wabunge wengine wahame mimi siwezi kuwasemea, Kuhusu suala la nani atakuwa mpinzani wangu kwenye uchaguzi wa marudio bado sijajua maana mimi bado sijapitishwa kugombea tena na uteuzi utafanyika disemba 20,” amesema Mtolea
Hata hivyo, Novemba 15 mwaka huu, Abdallah Mtolea alitangaza kujivua nafasi yake ya Ubunge na kwa kile alichokidai kuchoshwa na mgogoro uliokuwa ukiendelea kwenye Chama cha Wananchi CUF ambapo baadaye alitangaza kujiunga Chama Cha Mapinduzi CCM.
-
Jafo awapa neno TARURA
-
NEC yatoa somo kwa wasimamizi wa uchaguzi
-
Uwekezaji katika sekta ya madini waongezeka