Mtoto aliyenusurika kuuawa baada ya kutekwa na kukatwa Koromeo wilayani Njombe mkoani humo Februari 9, 2019, Meshack Myonga (4), amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Mtoto huyo alitekwa na mtu asiyejulikana akiwa nyumbani kwa wazazi wake Mtaa wa Mji Mwema Wilayani Njombe, kisha kupelekwa msituni na kukatwa Koromeo kabla ya kuokolewa, na kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa ya Kibena-Njombe na baadaye  kuhamishiwa hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi.

Aidha, mama mzazi wa mtoto huyo, Rabia Mlelwa amesema kuwa alikwenda hospitalini hapo na mtoto huyo kisha kuingizwa kwenye chumba cha matibabu, lakini baaye aliitwa na madaktari na kuambiwa kuwa mtoto huyo tayari ameaga dunia.

”Wakati wanaingia naye ndani hawakuniambia lolote kuhusu maendeleo yake, lakini baadaye waliniita na kuniambia mwanangu amefariki dunia, wamesema Koromeo lake lilikuwa limekaa vibaya hivyo alikuwa mtu wa kufa muda wowote.”amesema mama huyo kwa huzuni kubwa

Hata hivyo, mama wa mtoto huyo aliyefariki dunia amesema kuwa alitakiwa kurudi katika hospitali hiyo kujua maendeleo ya mwanaye baada ya kukaa wiki mbili katika hospitali hiyo ya rufaa wakipatiwa matibabu.

“Jana Mkuu wa wilaya ya Njombe (Ruth Msafiri) alitoa gari lililotuleta Mbeya, lakini leo baada ya tukio hili ametaarifiwa hivyo ameamuru gari hilo lirudi tena kwa ajili ya kutuchukua kurudi kijijini Ngalanga (Njombe),” amesema.

 

Wizara ya Afya yatoa tamko kwa waganga wa Jadi mkoani Njombe
Dkt. Gwajima azitaka timu za Afya mikoani kujitathmini kiutendaji