Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemkaribisha Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15), mwenye matatizo ya ngozi, ambaye alifika Ikulu kwa ajili ya kumshukuru kwa msaada aliompatia wa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ya Jijini Dar es Salaam.
Rais Samia, alimuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza wakati wa Ziara yake ya kikazi Nyakanazi Mkoani Kagera tarehe Oktoba 16, 2022 na kuagiza apatiwe matibabu baada ya kuhangaika kwa muda mrefu.
Rais Samia akimsikiliza Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye ni mkazi wa Nyakanazi Mkoani Kagera, wa kwanza kulia ni Kaka wa mtoto huyo Saddam Mustapha Baranyikwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye alifika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumshukuru kwa msaada aliompatia wa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye ni mkazi wa Nyakanazi Mkoani Kagera. Mtoto huyo Hamimu alifika Ikulu kwa ajili ya kumshukuru Rais kwa msaada aliompatia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye alikuwa na shauku kubwa ya kumuona Mhe. Rais Samia. Pichani mtoto huyo akiwa haamini macho yake mara baada ya kugundua kuwa aliyekuwa anazungumza naye ni Mhe. Rais Samia, Ikulu Jijini Dar es Salaam.