Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego amesema ataandaa mafunzo maalumu ya ukakamavu kwa ajili ya watendaji wote wa serikali mkoani humo wakiongozwa na yeye mwenyewe kwa ajili ya kuwaweka imara viongozi hao.

Amesema kuwa wapo kuna baadhi ya watendaji ambao wanabweteka katika utendaji kazi, hivyo kupitia mafunzo hayo anaimani watapiga kwata la maendeleo kwa wananchi wanaowaongoza

“Viongozi wote nitawaandalia mafunzo maalumu, tukafungiane tukapige kwata na tukirudi tupige kwata la maendeleo, wale ambao walipita jeshini wao wataji-brush tu lakini lengo kubwa ni kwa wale ambao hawajapita jeshini,” amesema Dendego

Aidha, mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa tofauti na zoezi hilo dhamira yake nyingine ni  kubuni vazi la kizalendo la mkoa huo ambalo litavaliwa na viongozi wote wa serikali katika siku zote za kazi ili kuwarahisishia wananchi kuwatambua viongozi wao.

Hata hivyo, kwa upande wake Ofisa tarafa wa Mtwara mjini, Oktaviani Lepembile amesema kuwa amepokea kwa mikono miwili mapendekezo ya mkuu wa mkoa huo.

Hamad Rashid: Wanasiasa acheni kutoa kauli za kichochezi
Mwanri amtaka mkandarasi kuendana na kasi ya JPM