Serikali Mkoani Tabora imeiagiza Kampuni ya Jossam & co Ltd  kuhakikisha inakamilisha barabara ilizopewa za Uledi na Mwenge katika Manispaa ya Tabora hadi kufikia mwishoni mwa Mwezi Septemba mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri baada ya kutembelea ujenzi wa barabara hizo zinazojengwa katika Kata ya Uledi na Isevya ili kujionea maendeleo na kuhakikisha kama mjezni amezingatia upana na urefu ullioandikwa katika makubaliano ya mkataba.

Amesema kuwa kiasi cha shilingi milioni 700 zilizopangwa na  Manispaa ya Tabora kutumika kukamilisha mradi huo ni fedha nyingi ni vema Mkandarasi anayejenga mradi huo akahakikisha anajenga katika kiwango bora na kwa upana na urefu uliomo katika mkataba ili thamani ya pesa ionekane.

Hata hivyo, Amewaagiza Watendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanasimamia kwa karibu ujenzi wa barabara hizo unazingatia matakwa yaliyoelezwa katika Mkataba wa Ujenzi ili barabara hizo ziweze kutumika kwa muda mrefu bila kuharibika.

 

Mtwara kupigishwa kwata
Magazeti ya Tanzania leo Agosti 21, 2017