Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amesema kuwa jirani zake Afrika Kusini walikuwa na nafasi kubwa zaidi ya kumsaidia dhidi ya hatua iliyochukuliwa na jeshi la nchi hiyo hali iliyomlazimu kuondoka madarakani.
Akizungumzuka katika mahojiano ya hivi karibuni, Mugabe aliulizwa kama anadhani Afrika Kusini ambayo ilikuwa rafiki wake wa karibu haikumlinda ipasavyo, alisema anaamini hivyo. “Katika hali hiyo, nadhani ndiyo,” alijibu Mugabe.
“Afrika Kusini ingeweza kufanya kitu zaidi. Sio kwa kutuma jeshi lake, lakini kuingilia kati kimkakati,” alijibu Mugabe.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma alimtuma jijini Harare waziri wake wa ulinzi na usalama, saa chache baada ya jeshi kuingilia kati mgogoro wa madaraka ndani ya Zanu-Pf na Mugabe kushinikizwa kujiuzulu.
- Manara awananga wanaozibeza Simba na Yanga
- Video: Sura mpya kesi ya Babu Seya na mwanae, Watu wasiojulikana wavamia magereza
Katika mahojiano hayo ndani ya jumba lake la kifahari, Mugabe alielezea hatua ya kumuondoa madarakani kama mapinduzi ya kijeshi na kinyume cha katiba.