Kumekuwa na uvumi unaosambazwa katika mitandao ya kijamii kutoka kitengo cha Rais, Ikulu idara ya Mawasiliano ikidai kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeharifu wananchi wake kufungia mitandao ya kijamii nchini endapo itatumika vibaya.

Kufuatia habari hiyo iliyochapishwa tarehe 24, Machi 2018 ikitoa maelezo hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa mapema leo hii ameikanusha barua hiyo na kudai kuwa haijachapishwa na idara yake.

Na kuwasihi Watanzania kuipuuza habari hiyo kwani ni uvumi ambao hauna ukweli wowote, kwani Serikali haijatoa wa kuzungumzia swala hiyo.

Msigwa ameyasema hayo asubuhi ya leo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii na kusema taarifa hizo ni uzushi mtupu hazina ukweli wowote, uzushi huo umetengenezwa na wahalifu wa mtandao.

Leo (Machi 24, 2018) imesambazwa barua iliyokuwa inaonesha kutoka Ikulu ambayo imeandika taarifa za kuwa serikali inawaasa watanzania wote wanaotumia mitandao ya kijamii kuitumia kwa uangalifu na tija ili kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Semakafu atoa mwongozo umri wa mwanafunzi kujiunga kidato cha tano/sita, 2018
Mugabe ailaumu Afrika Kusini kung'olewa urais