Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven jana Jumanne amepata chanjo yake ya nyongeza ya UVIKO 19 kutokana na kuendelea kuongezka visa vya wagonjwa wa Corona nchini Uganda.
Kulingana na kauli yake, Museven alisema watu waliopata chanjo zote zinazotakiwa wanaweza kushindana na ugonjwa huo na kupigana na kirusi kipya cha Omicron ambacho kinatahadharishwa kuenea kwa kasi.
Rais huyo ambae amepata chanjo zote za ‘AtraZeneca’ alisema alishauriwa na daktari wake kuongeza dozi ya chanjo ya ‘Pfizer’ ili kuongeza kinga yake ya mwili ya kushindana na virusi hivyo ambavyo mpaka sasa watu 145,963 wameambukizwa nchini Uganda na watu 3,306 wamefariki tangu March 2020 ambapo ugonjwa huo uliingia kwa mara ya kwanza nchini humo.
“Madaktari wangu, Diana Atwine mbaye ni wwaziri wa afya na Dkt Magooba, afisa wa jeshi wamenipatia dozi yangu ya nyongeza. Atwine ameleta aina nyingine ya chanjo, amesema ili niwe na kinga imara natakiwa kupata chanjo aina tofauti na ile niliyopata mwanzo,” alisema Museven.
Rais Museven aliendelea kusema kuwa “kwa sababu mwanzo nilipata chanjo ya AtraZeneca mara mbili, sasa ninapata ya Pfizer. Wanasema kuchanganya chanjo sio tu ni sawa ila ni vizuri zaidi, na hii ni kuwakumbusha wote mnatakiwa kupata chanjo zote ili kujikinga.” Rais Museven.
Siku ya Jumatatu Januari 3, 2022 wizara ya afya ya Uganda ilitangaza kuwa na kesi mpya za Corona 1,423.