Muigizaji nyota wa Hollywood kutoka Kenya Lupita Nyong’o aamelazimika kujiondoa kwenye hafla ya kunadi filamu yake mpya ya The 355 baada ya kupatikana na maambukizi ya COVID-19.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Nyota huyo wa Black Panther, mwenye umri wa miaka 38, ameandika kuwa ameathirika licha ya kuwa alikuwa amechanjwa.

“Nimepima na kukutwa na virusi vya COVID-19,” “Nimechanjwa kikamilifu kwa sasa ninajitenga kwa kukaa mbali na watu lakini ninaamini nitakuwa mzima.” Amesema Lupita.

“Tafadhali nawasihi mfanye yote muwezayo ili kujilinda wewe na wengine dhidi ya gonjwa ili hatari” Alisisitiza Lupita.

Nchi ya Sudan yapewa onyo
Museven apata chanjo ya nyongeza ya Uviko 19