Kwa mara ya kwanza Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekituhumu Chama cha Siasa cha NUP kwa kuhusika na vitendo vya udaganyifu wa wizi wa kura katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Januari 14, 2021.
Museveni amesema madai ya Robert Kyagulanyi, ‘Bobi Wine’ kwamba ushindi wake katika uchaguzi mkuu ulichukuliwa na rais Museveni na kumtaka kurudisha maamuzi ya wananchi.
Katika hotuba yake usiku wa kuamkia leo Machi 15, Rais Museveni amedai kwamba chama cha NUP kilifanya udaganyifu mkubwa katika zoezi la uchaguzi mkuu wa rais na wabunge ndiyo sababu walipata kura hizo hasa katika Mkoa wa Kati na baadhi ya sehemu za mkoa wa Busoga na kumuonya Bobi Wine kuwa mipango yake anayopanga kufanya ya maandamano.
“Ni upande wa upinzani hususan kundi la Kyagulanyi ambao walifanya udaganyifu mkubwa kila mtu nchini Uganda anafahamu nani aliyeiba ni kundi la Kyagulanyi.
“Hizo kura wanazodai zaidi ya milioni tatu hazipo, kulikuwa na vitisho vilivyofanywa na wafasi wa NUP, na sasa wapinzani wanapanga kuzuia kuapishwa Rais, hawawezi, yoyote anayepanga jeshi litawakamata,” amesema Museveni.
Aidha, Museveni amemlaumu Bobi Wine kwa kuwashauri vijana kufanya vitendo vya uhalifu, na kwamba hiyo ndiyo sababu iliyopelekea vijana hao kuwekwa mbaroni na vyombo vya usalama.