Watu 46 wamefariki dunia kufuatia mvua kali zilizonyesha nchini Brazil na kupelekea maporomoko ya ardhi ambayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu.
Mvua hizo zimenyesha siku ya Ijumaa na kudumu kwa muda wa masaa 24 na kupelekea idadi hiyo ya watu kufariki dunia huku wnegine kuokolewa na wengine 28 kupotea hadi sasa hawafahamiki walipo na majumba zaidi ya 20 kwenda na maji.
Kiongozi wa kitengo kinachohusika na usalama wa rais katika eneo la Minas Gerais amewatahadharisha wakazi wa maeneo tofauti na mvua kali ambazo zimeripotiwa kuendelea kunyesha.
Kwa ujumla watu 46 wamefariki nchini humo ambapo 9 wameripotiwa kufariki katika jimbo la Minas Gerais na 37 katika eneo la Espirito Santo.
Siku tatu za maombolezo zimetangazwa katika jimbo la Minas Gerais na katika miji mingine 47 kuomboleza vifo vya watu hao.