Mvutano mkubwa umetokea kuhusu mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Buyungu, kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA), Kasuku Bilago, huku kila upande ukipanga tarehe yake.
Katika ratiba iliyotolewa na Bunge imesema kuwa Bilago anatarajiwa kuzikwa kesho tarehe 30/ Mei 2018 mkoani Kigoma, lakini chama chake kimedai kuwa atazikwa keshokutwa.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Stephen Kagaigai amesema kuwa ratiba iliyotolewa na bunge ndiyo sahihi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa mwili wa marehemu Bilago utazikwa keshokutwa mkoani Kigoma.
“Labda waulize Bunge wanazika kesho mwili wa nani, wamewasiliana na chama gani au familia gani, sisi tunazika keshokutwa na tutaondoka mara baada ya kuaga hapo bungeni,”amesema Mbowe
Hata hivyo, Wabunge wa Chadema wamegoma kupanda gari lililoandaliwa na bunge kuwapeleka Kigoma kwa ajili ya kuhudhuria mazishi, huku wakidai kuwa wamekodi basi lao, hivyo basi la bunge litabeba wabunge wa CCM.
-
Dk. Saleh Ali Sheikh asifu amani na upendo wa Watanzania, “Ni mfano wa kuigwa na nchi nyingine”
-
Ratiba kamili safari ya mwisho ya Marehemu Bilago
-
Dkt. Hellen Kijo-Bisimba aachia ngazi LHRC