Wataalamu wa Umoja wa Mataifa, wamelaani sera ya Serikali ya Libya ya kuwazuia Wanawake kusafiri nje ya nchi bila kuandamana na mwanamume.

Hatua hiyo, ilipitishwa takriban miezi mitatu iliyopita na Serikali ya Abdel Hamid Dbeibah, yenye makao yake mjini Tripoli mashariki mwa Libya ambapo inaelekeza kuwa wale watakaokataa au kukiuka basi watapigwa marufuku kuondoka nchini humo.

Waziri Mkuu wa Libya Abdel Hamid Dbeibah, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Tripoli, Februari 25, 2021. Picha ya Hazem Ahmed/ AP.

Sheria hiyo mpya, iliyochukuliwa chini ya shinikizo kutoka kwa wanamgambo wa Kiislam wenye msimamo mkali wa dinihuko Tripoli, inawalazimisha wanawake na wasichana kuwa na mwanamume, anayeitwa “mahram”, ili waweze kusafiri na kujaza fomu ya kina inayobainisha sababu za safari yao.

Serikali ya Dbeibah ilitakiwa kutoa maelezo kwa wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa kuhusu hatua hiyo na shutuma hizo zinakuja baada ya siku 60, wakisema zinapinga haki za kimsingi na uhuru wa wanawake na wasichana.

Vijana acheni kuuza figo - Dkt. Mpango
Mkandarasi aliyeokoa Mil. 120 azawadiwa Milioni moja